Loading...

Michelle Obama ashindwa kujizuia kwa Beyonce



Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama amempa maua yake mwanamuziki Beyonce kwa kuvunja rekodi na kuweka historia na kubadilisha muziki kupitia Album yake mpya ya Cowboy Carter.

“Beyonce wewe ni mvunja rekodi na muweka historia. Ukiwa na Cowboy Carter, umebadilisha game kwa mara nyingine tena kwa kusaidia kufafanua upya aina ya muziki na kubadilisha utamaduni wetu. Ninajivunia wewe”

“Album hii inatukumbusha kuwa sote tuna uwezo. Kuna nguvu katika historia yetu, furaha yetu, kura zetu na kila mmoja wetu anaweza kutumia vipawa na talanta zetu ili kufanya sauti zetu zisikike kuhusu masuala muhimu sana kwetu”.

Cowboy Carter ni Album ya 8 studio ya Beyonce ambayo imetoka Machi 29, 2024 ikiwa na mikwaju 27.

Chanzo: Eatv
Michelle Obama ashindwa kujizuia kwa Beyonce Michelle Obama ashindwa kujizuia kwa Beyonce Reviewed by Zero Degree on 4/04/2024 05:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.