Mkuu wa Gereza akerwa wafungwa msamaha wa Rais kurudi gerezani
MKUU wa Gereza Kuu la Isanga mkoani Dodoma, ACP Zefania Neligwa, amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya wafungwa ambao wamekuwa wakipata msamaha wa Rais, lakini baada ya kipindi kifupi wanarejea magerezani kwa uhalifu. MKUU wa Gereza Kuu la Isanga mkoani Dodoma, ACP Zefania Neligwa, amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya wafungwa ambao wamekuwa wakipata msamaha wa Rais, lakini baada ya kipindi kifupi wanarejea magerezani kwa uhalifu.
Aliyasema hayo jana baada ya kupokea msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodona kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA).
Msaada huo ulitolewa kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa gereza la wanaume na wanawake Isanga kwa malengo ya kufuturu katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa na utaratibu wa kuwaachia wafungwa kwenye kila sherehe za kitaifa, lakini baadhi yao wamekuwa wakirejea tena tabia ambayo imekuwa ikikera na kuhuzunisha kwa kuwa msamaha huo walitakiwa kujirekebisha kitabia.
Alisema magereza yamekuwa sehemu kubwa ya kuwafanya watu wanaochukuliwa hatua za kisheria na kufungwa kuwa eneo la kujirekebisha tabia ili wanapoachiwa na msamaha au kumaliza kifungo wawe raia wema kwa jamii.
"Inapofikia hatua ya kuachiwa kwa msamahaa au kumaliza kifungo chake mimi pamoja na uongozi mzima wa magereza tumekuwa tukiwapa nasaha za kuwafanya wanaporudi huko majumbani waweze kuwa raia waliojifunza kitabia na wanatakiwa kutumia fursa walizojifunza kwa maendeleao.
Shekhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu aliwataka wafungwa na mahabusu walioko magerezani kutumia vyema mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya kutubu na kuomba toba ya kweli ili Mungu awasamehe katika adhabu zinazowakabili.
Shekhe Rajab alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani ni muhimu wafungwa na mahabusu waliofunga wakafuturu na kupata chakula kama ambavyo waliopo uraiani.
Naye Mwenyekiti wa BAKWATA, Wilaya ya Dodoma, Bashiru Omary alisema mahitaji hayo yaliyokabidhiwa wanaamini yataenda kuwasaidia wale ambao wamefunga kwa mwezi huu Ramadhani na hata ambao hawajafunga.
Hata hivyo, alitaja misaada hiyo iliyokabidhiwa kwa wafungwa na mahabusu kwenye gereza hilo kuwa ni pamoja na sukari, ndizi, viazi mviringo na vitamu, mavazi maharagwe na vitabu vya kujisomea.

Chanzo: Nipashe
Mkuu wa Gereza akerwa wafungwa msamaha wa Rais kurudi gerezani
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2024 07:05:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2024 07:05:00 AM
Rating: