Real, Bayern zatinga nusu fainali UEFA, City, Arsenal zafungasha
TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa penalti 4-3 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City kufuatia sare ya 1-1 usiku huu Uwanja wa Jijini Etihad Jijini Manchester.
Kwa upande mwingine, wenyeji, Bayern Munich wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal ya England usiku huu Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
Dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, mshambuliaji Mbrazil, Rodrigo Silva de Goes akianza kuifungia Real Madrid dakika ya 12, kabla ya kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne kuisawazishia Manchester City dakika ya 76.
Matokeo hayo yakafanya sare ya jumla 4-4 kufuatia Real Madrid nayo kulazimishwa sare ya 3-3 nyumbani.
Baada ya dakika 120, kwenye mikwaju ya penalti waliofunga za Real Madrid ni Jude Bellingham, Lucas Vázquez, José Ignacio Fernández ‘Nacho’ na Antonio Rüdiger, wakati Luka Modrić pekee alikosa.
Waliofunga za Manchester City ni Julián Álvarez, Philip Foden na Ederson Santana de Moraes, huku Bernardo Silva na Mateo Kovačić wakikosa.
Sasa Real Madird itakutana na Bayern Munich ambayo imeitoa Arsenal.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Joshua Walter Kimmich dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya beki Mreno, mzaliwa wa Ufaransa, Raphaël Guerreiro.
Bayern Munich wanatinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 9 Uwanja Emirates Jijini London.
Sasa Bayern Munich watakutana na mshindi kati ya Real Madrid na mabingwa watetezi, Manchester City katika Nusu Fainali Aprili 30 Ujerumani na marudiano Mei 7 ugenini.
Real, Bayern zatinga nusu fainali UEFA, City, Arsenal zafungasha
Reviewed by Zero Degree
on
4/18/2024 08:00:00 AM
Rating:
