Loading...

Tanzania yapewa hekta 60 Congo kujenga bandari kavu

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara (mwenye suruali nyeusi), akifafanua jambo mbele ya wataalam wa wizara hiyo na kutoka Lubumbashi, Congo, mara baada ya kuonyeshwa eneo la ekari 60 ambalo Tanzania imepewa kwa ajili ya kujenga Bandari

SERIKALI ya Congo imekamilisha taratibu za awali za kuipatia ardhi Tanzania yenye ukubwa wa hekta 60 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa bandari kavu katika nje kidogo ya mji wa Lubumbashi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, baada ya makubaliano ya awali hatua ya kusaini itafanyika Juni mwaka huu.

Kiongozi huyo aliambatana na timu ya watalamu kutoka serikali na Mamlaka ya Bandari TPA katika kikao kilichofanyika mjini Lubumbashi DRC Aprili 26 na 27 mwaka huu.

Prof. Kahyarara alisema makubalino ya utekelezaji wa mradi huo yatafanyika katika kikao cha mawaziri wa sekta za uchukuzi chini ya Ushoroba wa Kati- CCTTFA mjini Lubumbashi.

Aidha, alieleza umuhimu wa DRC kutumia bandari za Tanzania hasa ya Dar es Salaam ni mkubwa kwa kuwa ndio inaongoza kwa kupitisha bidhaa zake kutokana na sera nzuri za uchumi wa kidiplomasia na kuifungua nchi kunakofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Pro. Kahyarara shehena inayokwenda DRC imeongezeka kwa asilimia 189 kutoka tani milioni 1.8 hadi tani milioni 3.4 katika kipindi cha miaka mitatu.

Aidha, alisema serikali imejiwekea mikakati ya kuongeza shehena inayopita kwenye bandari zake na kuiomba DRC kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kama lango lake kuu.

Chanzo: IPPmedia
Tanzania yapewa hekta 60 Congo kujenga bandari kavu Tanzania yapewa hekta 60 Congo kujenga bandari kavu Reviewed by Zero Degree on 4/29/2024 08:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.