Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Aprili, 2024

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane

Meneja wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane anafuatilia kwa karibu hali ya meneja wa Manchester United, Erik ten Hag na angependelea kuinoa klabu hiyo ya Old Trafford badala ya Bayern Munich. (L'Equipe)

Bayern Munich haijawasiliana na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Zidane kuhusu kumrithi Thomas Tuchel, ambaye anaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)

Aliyekuwa mkufunzi wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick, ambaye ni meneja wa Austria, amejadiliwa na uongozi wa Bayern , huku kocha wa Brighton Roberto de Zerbi pia akiwa kwenye orodha yao ya watu wanaoweza kuwania nafasi hiyo. (Sky Sport Germany)

Kiungo wa kati wa Newcastle United na timu ya taifa ya Brazil Bruno Guimaraes, 26, amedokeza kuwa ana nia ya kusalia katika klabu hiyo msimu ujao baada ya kununua nyumba mpya Kaskazini Mashariki.(Telegraph)

Beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 22, ameiambia Chelsea kwamba anataka kuondoka huko na ana nia ya kusalia Dortmund, ambako yupo kwa mkopo. (Sky Sport Germany)

Manchester United wanakabiliwa na ushindani kutoka klabu ya Atletico Madrid kuwania saini ya beki wa kati wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24. (Mirror).

Jadon Sancho

Manchester United inaweza kuwa katika mstari wa kupokea pauni milioni 3.4 za ziada kwa ajili ya mkopo wa winga wa Uingereza Jadon Sancho kwenda Borussia Dortmund ikiwa timu hiyo ya Ujerumani itatinga fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Times)

Bayern Munich wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 26 , ambaye anaweza kugharimu kati ya Euro 60-70m.(Relevo)

Fulham wako tayar kwa ajili ya ofa ya mshambuliaji wa Brazil Carlos Vinicius, 29, ambaye ana mkataba wa mkopo katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki ya Super Lig hadi mwisho wa msimu. (Standard)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/20/2024 09:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.