Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Aprili, 2024
Mohamed Salah anatarajiwa kuwaniwa na vilabu vya Saudi Pro League tena msimu huu wa joto huku Al-Ittihad wakijiandaa kutoa pauni milioni 70 kwa mshambuliaji huyo wa miaka 31 wa Liverpool na Misri. (Talksport)
Manchester City wamekubaliana na kiungo wa West Ham Lucas Paqueta kabla ya uhamisho wa majira ya joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 26, alihusishwa pakubwa na kuhamia Etihad Stadium mwaka jana. (Foot Mercato)
Klabu ya Liverpool wamempa meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp huko Anfield. (Pedro Sepulveda)
West Ham wameungana na Liverpool , Tottenham na AC Milan katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Fulham Tosin Adarabioyo, 26, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu wa joto.(Guardian)
Chelsea inapaswa kuwavutia kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 29, na mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 26, kuondoka Manchester United msimu huu wa joto, kulingana na mlinzi wa zamani wa Blues William Gallas. (Mirror)
Chelsea hawana nia ya kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Athletico Paranaense Bento, 24, lakini Inter Milan wanatazamiwa kukabiliwa na ushindani kutoka kwingineko kwenye Ligi kuu ya Uingereza kwa mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil. (Gazetto dello Sport)
Borussia Dortmund wana nia ya kumsajili winga wa PSV Eindhoven, Johan Bakayoko, 20 . Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji pia anaripotiwa kulengwa na vilabu vya Burnley na Brentford . (Voetbal International)
Beki wa Everton na England Jarrad Branthwaite anasema anazuia kelele kuhusu mustakabali wake huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akivutia Manchester United na Real Madrid .(90min)
Chelsea wanajaribu kuwapiku wapinzani wao na kutoa ofa ya pauni milioni 43 kwa mshambuliaji wa Athletic Bilbao Nico Williams, 21, kabla ya dirisha la uhamisho kufunguliwa.
The Toffees pia wanaweza kutarajia ofa kwa kiungo wa Ubelgiji Amadou Onana hukuAfisa mkuu mtendaji wa zamani wa Everton Keith Wyness akisema klabu hiyo inaweza kupata hadi £70m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 huku Arsenal , Newcastle United na West Ham wakimtaka. (Football Insider)
Paris St-Germain hawajakata tamaa katika kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Barcelona na Uhispania Gavi msimu huu wa joto licha ya kifungu cha kutolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kuwa euro bilioni moja. (L'Equipe)
Kiungo wa zamani wa klabu ya West Ham Felipe Anderson anakaribia kukubali dili la kujiunga na Juventus kama mchezaji huru. Mkataba wa winga huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 huko Lazio unamalizika mwishoni mwa msimu. ( Fabrizio Romano)
Mkufunzi wa Real Betis Manuel Pellegrini hajakutana na maafisa kutoka Roma kuhusu kuchukua nafasi ya ukocha katika uwanja wa Stadio Olimpico huku Mchile huyo mwenye umri wa miaka 70 akitembelea mji mkuu wa Italia hivi majuzi kwa likizo ya kifamilia. (Muchodeporte)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Aprili, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2024 08:29:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/09/2024 08:29:00 AM
Rating:

.jpeg)