Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Aprili, 2024


Manchester City wanataka kumzawadia Rodri nyongeza ya mshahara ambayo itamfanya kiungo huyo wa kati wa timu ya taifa ya Uhispania, 27, abaki na klabu hiyo katika maisha yake yote ya soka. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza Kalvin Phillips, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo West Ham, amepangwa kama mmoja wa walengwa wa Fulham msumu ujao. (Football Transfers).

Phillips anaweza kujiunga tena na klabu ya kwao Leeds United ikiwa wako tayari kulipa £30-£40m. 

Liverpool wako kwenye mazungumzo na Trent Alexander-Arnold kuhusu mkataba mpya wa beki huyo wa kulia wa Uingereza, 25.


Kipa wa England Aaron Ramsdale anatarajiwa kuondoka Arsenal msimu huu, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akilengwa na Newcastle United. (Football Insider)

Arsenal na Chelsea wanavutiwa na Viktor Gyokeres lakini Sporting Lisbon hawatakubali chini ya euro 100m (£85.8m) kwa mshambuliaji huyo wa Uswidi, 25. (Pedro Sepulveda).

Atletico Madrid wanavutiwa na kiungo wa kati wa Fulham wa Brazil Andreas Pereira, 28. (Sky Sports)

Bodi ya klabu ya Manchester United itasubiri hadi mwisho wa msimu kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa meneja wake Erik ten Hag, licha ya kuwapo shinikizo kwenye nafasi ya Mholanzi huyo. (Times)

Manchester United wana nia ya kumteua kocha wa Bologna Thiago Motta kama mbadala wa Ten Hag. (Gazzetta dello Sport)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Everton Frank Lampard ameibuka kuwa mgombea wa kushtukiza kuchukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Canada. (Telegraph)

Dinamo Zagreb wamelipa tangazo la ukurasa mzima katika gazeti la michezo linalouzwa zaidi nchini Uhispania, Marca, katika jaribio la kumshawishi kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 38, kurejea katika klabu yake ya kwanza iwapo ataamua kuondoka Real Madrid msimu huu. (ESPN)

Paris St-Germain wamesitisha mazungumzo ya kuongeza mkataba na mdogo wake Kylian Mbappe, Ethan Mbappe, 17, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa chini ya miaka 16 ukimalizika Juni. (RMC Sport)


Sevilla watataka kumuuza mfungaji bora Youssef En-Nesyri, huku mshambuliaji huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 26 akiwa "mlengwa" katika vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia. (Marca)

Arsenal wameungana na Manchester United pamoja na Bayern Munich kumfuata Mikayil Faye wa Barcelona kabla ya kumnunua beki huyo wa Senegal, 19. (Mail).
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/07/2024 08:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.