Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Aprili, 2024

Jadon Sancho, 24

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, atakuwa tayari kurejea na kucheza tena soka yake katika klabu ya Manchester United iwapo meneja Erik ten Hag ataondoka. (News)

Arsenal wanatarajiwa kufufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa klabu ya Aston Villa na timu ya taifa ya Brazil Douglas Luiz, 25, msimu huu. (Football Insider)

Manchester United wameelekeza mawazo yao kwa beki wa Nice mwenye umri wa miaka 24 Jean-Clair Todibo baada ya kupunguziwa bei ya kumsajili beki wa kati wa Everton, 21, Jarrad Branthwaite.

Klabu ya Fulham imeweka kipaumbele kumsajili Trevoh Chalobah wa Chelsea, 24, kama mbadala wa mlinzi mwenzake wa kati Tosin Adarabioyo, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (TeamTalks)

United wanataka kumuuza winga wa Brazil Antony, 24, msimu ujao (Rudy Galetti)

Klabu ya Bayer Leverkusen wameweka bei ya euro 150m (£128m) kwa kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz mwenye umri wa miaka 20 huku Barcelona na Real Madrid wakimtaka. (Radio Marca)

Arsenal na Liverpool wanavutiwa na beki wa kati wa Ecuador Willian Pacho, 22, anayechezea Eintracht Frankfurt. (Florian Plettenberg)

Kobbie Mainoo, 18

Manchester United itaanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18 kuhusu kandarasi mpya msimu ujao. (Sun)

Arsenal itamfanya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Eddie Nketiah, 24, kupatikana kwa uhamisho msimu huu wa joto lakini wataomba £40m. (HITC)

Tottenham wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Giorgi Sudakov, 21. (Offside)

Everton wana nia ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Newcastle wameanzisha upya nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa klabu ya Nottingham Forest, raia wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 24. (Football Insider)

Liverpool wanatazamiwa kumteua David Woodfine kama mkurugenzi msaidizi wa michezo wa Richard Hughes, baada ya kurejea Anfield chini ya mwaka mmoja baada ya kuihama klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Arthur Okonkwo, 22

Wrexham wanataka kubadilisha mkopo wa mlinda lango wa Uingereza, Arthur Okonkwo, 22 kutoka klabu ya Arsenal kuwa mkataba wa kudumu. (Subscription Required)

Juventus itasikiliza ofa kwa fowadi wa Italia Federico Chiesa, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Newcastle, baada ya kutofautiana kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na bosi Massimiliano Allegri kuhusu jukumu lake. (Tuttosport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/17/2024 10:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.