Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Aprili, 2024


Inter Milan wanaweza kumnunua fowadi wa Ufaransa Anthony Martial wakati kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na Manchester United itakapokamilika msimu huu wa majira ya joto - ikiwa watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Iceland Albert Gudmundsson, 26, kutoka Genoa.

Winga wa Italia Nicolo Zaniolo anataka kurejea Serie A wakati mkopo wake kutoka Galatasaray kwenda Aston Villa utakapomalizika msimu huu, huku Fiorentina na Napoli wakiwa tayari wameulizia kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport)

Brighton hawana nia ya kumnunua tena Ansu Fati baada ya uhamisho wake wa mkopo kutoka Barcelona lakini Wolves , Valencia na Sevilla wanawezakuwasilisha ofa kwa mshambuliaji huyo wa Uhispania, 21 msimu huu wa joto. (Sport).

Vilabu vya Bundesliga vina nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 22 kutoka Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, ambaye amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Excelsior ya Uholanzi msimu huu.

GETTY IMAGES

Amadou Onana huenda akaondoka Everton msimu huu wa joto, huku The Toffees wakitumai kupokea pauni milioni 50-60 kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji, 22. 

Klabu ya Everton itahitaji zaidi ya pauni milioni 40 ili kumuuza mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Luton wameonyesha nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Blackburn na Jamhuri ya Ireland Sammie Szmodics lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Brentford (Sun)

Beki wa timu ya taifa ya Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, anasisitiza kuwa anazingatia zaidi kushinda mechi na Everton na kwamba anapuuza uvumi wote kuhusu mustakabali wake wa muda mrefu, baada ya kuhusishwa na Manchester United. (Liverpool Echo)

Juventus wamefikia makubaliano kimsingi na Thiago Motta kwa bosi wa Bologna kuwa kocha wao mpya - na kiungo wa kati wa Bologna na Scotland Lewis Ferguson, 24, anaweza kumfuata Turin. (Calciomercato)

Manchester United wameimarisha nia yao ya kumnunua Miguel Gutierrez wa Girona na wanatazamia kushinda Arsenal katika kumsajili beki huyo wa kushoto wa Uhispania, 22, msimu huu. (Mirror)


Real Madrid wanamtazama kiungo wa River Plate Muargentina Franco Mastantuono, 16, ambaye pia anafuatiliwa na Chelsea na Paris St-Germain . (Fabrizio Romano)

Barcelona na Manchester City pia wanavutiwa na Mastantuono, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 45m (pauni 38.6m). (Sport)

Klabu ya Manchester United wamewasiliana na klabu ya Palmeiras kuhusu mshambuliaji wa Brazil Thalys, 19, ambaye bado hajacheza kwa mara ya kwanza katika kikosi chake cha kwanza. (TeamTalk)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/08/2024 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.