NBCPL: Hatutakiwi kupoteza michezo iliyobaki - Thabit
UONGOZI wa Azam FC umesema licha ya kuhitaji pointi tatu ili kumaliza ligi ikiwa katika nafasi mbili za juu, lengo lao lingine kubwa ni kulipa kisasi dhidi ya Namungo kutokana na kupoteza mechi ya nyumbani ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Oktoba 27, mwaka jana Azam ikiwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Namungo.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Azam, Thabit Zacharia, alisema moja kati ya mechi muhimu zaidi msimu huu kwao katika Ligi Kuu Bara ni dhidi ya Namungo itakayochezwa keshokutwa mkoani Lindi.
Zaka alisema mbali na kuhitaji pointi tatu kutokana na vita kali iliyopo juu kati yao na vigogo, Simba na Yanga, lakini wanahitaji kulipiza kisasi kwa sababu hawaelewi sababu iliyofanya wakafungwa katika mechi wa kwanza.
"Ni mchezo muhimu kwetu japo tupo juu ya Simba, lakini tuko huko kwa sababu tumecheza michezo mingi zaidi, hivyo hatutakiwi kupoteza michezo iliyobaki, hatutakiwi kuangusha pointi zaidi kwa sababu kuna wenzetu tumewazidi lakini wana michezo michache.
Halafu kisasi ni haki, tunakwenda kulipiza kisasi kwa sababu mchezo wa kwanza walitufunga hapa kwetu Azam Complex," alisema Zaka Zakazi.
Azam FC inakwenda kucheza mechi hiyo ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo, ikiwa na pointi 47, nyumba ya Yanga inayoongoza kwa pointi 52 na juu ya Simba iliyo nafasi ya tatu yenye pointi 45.
Hata hivyo, Azam imecheza mechi mbili zaidi ukilinganisha na Simba, ikiwa imeshuka dimbani michezo 21, Wekundu wa Msimbazi wakicheza mechi 19 mpaka sasa.

Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2024 01:41:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2024 01:41:00 PM
Rating: