Watu 7 wafariki ajalini Singida
WATU saba wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa baadhi yao vibaya baada ya basi la Kampuni ya Luginga Express walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga lori la mizigo kwa nyuma ambalo lilikuwa limeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda,akizungumza na Nipashe Digital hili Leo kwa njia simu amesema ajali hiyo imetokea Leo saa 10:30 alfajiri katika kijiji cha Malendi kilichopo kata ya Mgongo wilayani humo.
Watu 7 wafariki ajalini Singida
Reviewed by Zero Degree
on
4/10/2024 02:20:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/10/2024 02:20:00 PM
Rating:
