Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 3 Mei, 2024

Michael Olise, 22

Klabu ya Manchester United wako mbioni kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Ufaransa chini ya umri wa miaka 22, Michael Olise. (ESPN)

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi asalia kwenye orodha ya kocha wa Bayern Munich baada ya Ralf Rangnick kukataa ofa ya klabu hiyo ya Ujerumani. (Bild)

Juventus wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mashambuliaji wa Manchester United na Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe ya Uhispania. (i Sport)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva

Kocha wa Barcelona Xavi ameiambia klabu hiyo kwamba anamtaka kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, lakini Bayern Munich pia wanamtaka. (Sport)

Chelsea wanafikiria kumnunua mlinda lango wa Poland Wojciech Szczesny, 34 - mlinda mlango wa zamani wa Arsenal ambaye sasa anachezea Juventus. (Tutto Juve)

Chelsea wameungana na Newcastle kuulizia hali ya mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 26, ambaye ataondoka Fulham kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Beki wa Borussia Dortmund Mholanzi Ian Maatsen

Manchester City walikuwa miongoni mwa timu zilizomchunguza beki wa Borussia Dortmund Mholanzi Ian Maatsen, 22. (TBR Football)

Villa wanataka kumsajili shambuliaji wa Leicester na Nigeria Kelechi Iheanacho, 27, kama mshambuliaji msaidizi wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Ollie Watkins, 28.

Leicester City wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Coventry City Muingereza Callum O'Hare, 26. (Football Insider)

Beki wa kati wa Aston Villa na Brazil Diego Carlos, 31, ni mmoja wa walengwa wakuu wa AC Milan. (Team Talk)

Gabriel Jesus yuko tayari kupigania nafasi yake katika klabu ya Arsenal

Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 27, yuko tayari kupigania nafasi yake katika klabu ya Arsenal huku kukiwa na tetesi zinazoashiria mchezji huyo anaweza kuondoka majira ya kiangazi. (Sun)

Brighton, Fulham, West Ham na Benfica wanamfuatilia winga wa Vitoria de Guimaraes na Ureno Jota Silva, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 17. (Rudy Galetti)

Inter Miami wameanza mazungumzo na winga wa Benfica mwenye umri wa miaka 36 na Argentina Angel di Maria. (ESPN Ajentina)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 3 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 3 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/03/2024 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.