Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Mei, 2024

Thomas Tuchel

Kocha wa zamani wa klabu ya Bayern Munich na Chelsea Thomas Tuchel ni miongoni mwa orodha ya makocha wanaowaniwa na klabu ya Manchester United kuchukua nafasi ya Erik ten Hag iwapo Mholanzi huyo ataondoka msimu huu wa majira ya joto. (Times)

Lakini Thomas Tuchel amefungua milango ya kusalia Bayern Munich baada ya msimu huu licha ya kutangazwa Februari kwamba ataondoka. (Florian Plettenburg)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amemfanya mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 24, kuwa shabaha yake kuu msimu huu wa joto. (Independent)

Everton wanatumani ya kumshawishi Jarrad Branthwaite, 21, kusalia Goodison Park kwa mwaka mmoja zaidi lakini Manchester United wana imani kwamba dau la £60-70m kwa beki huyo wa kati wa Uingereza litakubaliwa.

Klabu ya Arsenal wameanza mazungumzo ya kandarasi na mlinzi wa kati wa Brazil Gabriel, 26, katika jitihada za kupigana na klabu kubwa za Ulaya. (Football Insider)

Makamu wa rais wa Inter Milan Javier Zanetti amependekeza kuwa mabingwa hao wa Serie A huenda wakashindana na Manchester United na Arsenal katika kuinasa saini ya mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Klabu ya Manchester United imefanya mawasiliano na wakala wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye mkataba wake na Juventus unakamilika msimu huu wa joto. (Team Talk)

Mlinzi wa kati wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, anaelekea kujiunga na Newcastle mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Mail)

Richarlison, 26 

Klabu ya Tottenham itasikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 26 msimu huu wa joto. (Telegraph)

Real Madrid imefanya uchunguzi kwa River Plate kuhusu kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa chini ya miaka 20, Franco Mastantuono, 16. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Barcelona wamemfanya kiungo wa kati wa Arsenal na timu ya taifa ya Ghana Thomas Partey, 30, kuwa mlengwa wao mkuu katika usajili msimu huu. (Caught offside)

Klabu ya Manchester City wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Lazio Christos Mandas, huku Manchester United pia ikimtaka mlinda mlango huyo wa timu ya taifa ya Ugiriki mwenye umri wa miaka 22. (Corriere dello Sport)

Inter Miami wako kwenye mazungumzo ya kumleta kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid na Argentina Angel Di Maria, 36, kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Soka. (ESPN Argentina)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/04/2024 12:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.