Loading...

Serikali yasitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki za wafanyabiashara wa Kariakoo


Serikali ya Tanzania imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania nchini humo (TRA) katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam.

Zoezi hilo limesitishwa wakati utaratibu mzuri ukiandaliwa wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, ameyasema hayo wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya viongozi wa wafanyabiashara Tanzania, viongozi wa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

Kabla ya tangazo hilo maduka mengi katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania yalifungwaleokutokana na kile kinachosemekana kuwa mgomo wa wafanyabiashara wakishinikiza serikali kutekeleza madai yao.

Pamoja na madai mengine, wafanyabiashara hao walitaka kuondolewa kwa baadhi ya tozo na kodi na kukamatwa kiholela na mamlaka hasa za ukusanyaji kodi.
Serikali yasitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki za wafanyabiashara wa Kariakoo Serikali yasitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki za wafanyabiashara wa Kariakoo Reviewed by Zero Degree on 6/25/2024 07:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.