Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 15 Juni, 2024

Michael Olise, 22

Chelsea wamekubaliana kwa maneno na winga wa chini ya miaka 21 wa Crystal Palace na Ufaransa Michael Olise, 22, na wanatazamiwa kulipa ili kupata uwezekano wa kupata mkataba huo. (Team Talk)

Arsenal imetangaza bei yao ya mchezaji Emile Smith Rowe ya £30m , huku Reiss Nelson akiwafahamisha Gunners kuhusu nia yake ya kupima chaguo lake, Chelsea wanapewa ruhusa ya kuzungumza na Jhon Duran.

Arsenal wako tayari kukubali dau la pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 23, msimu huu.

Manchester City haitakubali ofa zozote kwa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 24, msimu huu wa joto.

Newcastle wamefanya mawasiliano na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Uingereza Fikayo Tomori, 26. (Football Insider)

Winga wa Uingereza Reiss Nelson, 24, ameifahamisha Arsenal kwamba anataka kutathmini chaguo lake kuhusu uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo. (Athletic)

Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ana kibarua kipya cha kutoa tathmini ya kiufundi kwenye mechi za Euro msimu huu wa Uefa.

Everton wameungana na Tottenham , Aston Villa na West Ham kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Roma Mwingereza Tammy Abraham, 26. (Mail)

Nico Williams, 21

Klabu ya Arsenal inamuwinda winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 21, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 50m (£42.2m). (Football London)


Chelsea imepewa ruhusa na Aston Villa kujadili masuala ya kibinafsi na mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20. (Telegraph)

The Blues , hata hivyo, hawana uhakika kama wanataka kuendelea na mpango wa kumnunua Duran (Guardian)

Villa pia wamefanya uchunguzi na Chelsea kuhusu beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 22, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Borussia Dortmund. (Sky Sports)

Klabu ya Manchester United wako tayari kutafuta safu nyingine ya ulinzi ikiwa Everton hawako tayari kufanya mazungumzo ya kumnunua beki wa kati wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21. (ESPN)

Fabian Hurzeler

Brighton wanatazamiwa kumteua Fabian Hurzeler kama meneja wao mpya baada ya kukubali kulipwa fidia na klabu ya St Pauli ya Ujerumani. (Fabrizio Romano)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 15 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 15 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/15/2024 08:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.