Loading...

Djuma ajiunga na klabu ya Namungo

Aliyekuwa beki wa Yanga, Djuma Shaaban

Klabu ya Namungo, imetangaza kumsajili beki wa zamani wa Yanga na AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Djuma Shaaban, ambaye ataitumikia timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano mbalimbali, ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, imeeleza usajili wa mchezaji huyo ni moja ya mapendekezo ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ili kukiboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao.

Imeeleza tayari mchezaji huyo ameshafika Rungwa mkoani Lindi na ameanza mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano.

Awali, beki huyo wa kulia alitajwa kuwa angejiunga na Coastal Union, ambapo Ofisa Habari wa klabu hiyo, Abbas El Sabri, alithibitisha kuwa walikuwa kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuisaidia timu yao katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mpaka anajiunga na timu hiyo, Djuma hakuwa na klabu yoyote, lakini aliichezea Yanga kuanzia 2021 hadi 2023, ambayo ilimsajili kutoka AS Vita Club ya DR Congo.

Mbali na mchezaji huyo, Namungo pia imetangaza kupata saini wa kiungo wa zamani wa Yanga, Rafael Daudi Loti na Mubarak Amza Ngamchiya, wote kutoka Singida Fountain Gate.

Msimu uliopita Namungo ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya sita, kwa pointi 36, ikicheza mechi 30, kushinda nane, sare 12 na kupoteza mechi 10, ikifunga mabao 27 na kuruhusu 29.
Djuma ajiunga na klabu ya Namungo Djuma ajiunga na klabu ya Namungo Reviewed by Zero Degree on 7/29/2024 11:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.