Loading...

Atupwa jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka 13 Rombo


Mahakama ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, mkazi wa Kijiji cha Mbomai, wilayani humo, Ally Mbwambo (41) kwa kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13.

Kesi hiyo ya ubakaji namba 14008/2023, ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Desemba 28, 2023, mbele ya Hakimu wa Wilaya hiyo, Innocent Nyella.

Inadaiwa Machi 14, 2023 mshitakiwa huyo kwa makusudi, alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 na kumsababishia maumivu makali.

Awali, akitoa hukumu hiyo jana Jumatano Agosti 7, 2024 Hakimu Nyella ameieleza mahakama hiyo wamejiridhisha na maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa pande zote kwamba mshitakiwa huyo pasi na shaka alimbaka mtoto huyo.

Hata hivyo, Hakimu Nyella amesema mshitakiwa huyo atatakiwa kutumika adhabu ya kifungo hicho cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia hiyo.
Atupwa jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka 13 Rombo Atupwa jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka 13 Rombo Reviewed by Zero Degree on 8/08/2024 07:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.