Loading...

Muogeleaji wa Slovakia azimia baada ya shindano kwenye Olimpiki


Muogeleaji wa Slovakia Tamara Potocka anapokea matibabu baada ya kuzirai kufuatia misururu ya kuogelea mita 200 katika uwanja wa La Defense Arena kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris.

Potocka, mwenye umri wa miaka 21, alianguka kando ya bwawa, ambapo alipokea huduma ya matibabu ya haraka ikiwa ni pamoja na kupewa oksijeni.

Timu ya Slovakia iliiambia BBC Sport kuwa Potocka ni mgonjwa wa pumu na alikuwa na shambulio la pumu.

Potocka ameweza kupata fahamu na aliweza kuwasiliana na madaktari. Amepelekwa hospitali kwa uangalizi zaidi wa matibabu.
Muogeleaji wa Slovakia azimia baada ya shindano kwenye Olimpiki Muogeleaji wa Slovakia azimia baada ya shindano kwenye Olimpiki Reviewed by Zero Degree on 8/02/2024 02:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.