Loading...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aapishwa


Spika wa Bunge, Dk.Tulia Ackson amemuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa 16 leo Agosti 27,2024, jijini Dodoma.

Mwanasheria huyo aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akichukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi ambae ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Johari ambaye ndiye atakuwa mshauri mkuu wa kisheria wa Serikali na Bunge, akisimamia masuala ya kisheria, kabla ya kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali aapishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali aapishwa Reviewed by Zero Degree on 8/27/2024 05:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.