Loading...

Treni ya abiria yapata ajali Kigoma, 70 wajeruhiwa


Shirika la Reli Tanzania (TRC ) limetoa taarifa kuwa treni ya abiria namba Y14 ikiwa na kichwa cha treni namba 9002, mabehewa 12 ya abiria, behewa moja la vifurushi (parcel) na behewa moja la breki imepata ajali kati ya Stesheni ya Kazuramimba na Uvinza mkoani Kigoma majira ya saa 7.30 usiku wa kuamkia leo Auguts 2024.

Taarifa iliyotolewa leo August 28,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk imesema

“Ajali imetokea baada ya mabehewa sita ya treni kuacha njia na kupelekea majeruhi 70, Wanawake 26 na Wanaume 44, treni ilikuwa na jumla ya abiria 571 wakisafiri kutoka Kigoma kuelekea Mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

“TRC kwa kushirikiana na Kitengo cha Afya cha Mkoa wa Kigoma walifanikiwa kuwapeleka majeruhi katika Hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwa ajili ya matibabu, hali za afya za abiria zinaendelea kuimarika, majeruhi 57 tayari wameruhusiwa, nane wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza na watano wamehamishiwa Hospitali ya Maweni kwaajili ya matibabu”

“Treni iliendelea na safari kuelekea Mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, Shirika linawapa pole majeruhi na linaendelea na jitihada za kuwahudumia, hakuna taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,”
Treni ya abiria yapata ajali Kigoma, 70 wajeruhiwa Treni ya abiria yapata ajali Kigoma, 70 wajeruhiwa Reviewed by Zero Degree on 8/29/2024 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.