Loading...

Simba haijapotea, msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya - Mo


"Najua mioyo yenu imebeba maswali mengi. Kama rais wenu, msione nimekaa kimya wakati tumepitia kipindi hiki kigumu. Kupambania Simba ni wajibu wangu. Huu sio wakati wa lawama ni wakati wa kisimam imara, kuwa kitu kimoja na kuchukua hatua sahihi kuleta mabadiliko chanya.

Katika siku chache zijazo nitazungumza nanyi moja kwa moja. Kuna kati kubwa inaendelea, na kuna matumaini ya kweli.

Simba haijapotea. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito - tumejenga kikosi kipya, tumeimarisha benchi la ufundi, na tumeweka msingi wa mwelekeo mpya. Msimu huu tumefika mbali zaidi ya matarajio na msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya.

Naomba tuendelee kuwa wavumilivu. Tunahutaji kufanya marekebisho makubwa. Tuendelee kusimama pamoja kama familia moja.

Mbele yetu kuna mwanga, na kwa pamoja tutarudi imara zaidi, wenye njaa zaidi na wakishujaa zaidi." - ameandika rais wa Simba SC, Mohamed Dewji.
Simba haijapotea, msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya - Mo Simba haijapotea, msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya  -  Mo Reviewed by Zero Degree on 7/11/2025 07:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.