Gombo wa Chama Cha Wananchi akabidhiwa fomu ya urais
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kupitia Mwenyekiti wake Jaji Jacobs Mwambegele, imemkabidhi mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Gombo Gombo, fomu za uteuzi kugombea nafasi hiyo.
Gombo amefuatana mgombea mwenza wake, Husna Abdalla, leo Agosti 13, 2025 katika ofisi za makao makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Njedengwa, Jijini Dodoma.
Viongozi hao wamesindikizwa na wanachama wa CUF kuchukua fomu hizo za uteuzi wa kugombea kiti cha Urais na Makamu wa Rais.
Chama Cha Wananchi (CUF), kimekuwa Chama cha 14 kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais na Makamu wa Rais katika Ofisi za Tume Huru za Uchaguzi (INEC), zilizopo Jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo, ameahidi kwamba endapo atachaguliwa kuwa rais, atasimamia haki na kuhakikisha rasilimali za Taifa zinawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi.

Reviewed by Zero Degree
on
8/13/2025 08:02:00 PM
Rating: