Loading...

Tanzania, Indonesia kuendeleza ushirikiano katika sekta ya kilimo


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Tri Yogo Jatmiko amesema Indonesia Itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Kilimo ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizoendelea zaidi kiteknolojia Duniani katika Sekta hiyo.

Mhe. Tri Yogo Jatmiko amesema hayo tarehe 2 Agosti 2025, katika uzinduzi wa Muongozo wa Shamba Darasa wa Kilimo Biashara katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane 2025, yanayofanyika Nzuguni, mkoani Dodoma.

Ameeleza kuwa Indonesia inatumia Teknolojia mbalimbali katika kilimo ikiwemo mawingu ya angani katika kuzalisha mvua ili iweze kutumika katika kilimo pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi.

Ameongeza kwa kusema ni muhimu kwa nchi kutengeneza masoko ya bidhaa za kilimo na kuwezesha uhitaji wa bidhaa husika katika masoko ya ndani na nje ya nchi kupitia teknolojia za kisasa, mbegu bora na miundombinu ya umwagiliaji.

Mhe. Balozi Tri Yogo Jatmiko amehitimisha kwa kuipongeza Wizara ya Kilimo kwa maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane 2025 yanayoendelea hapa nchini ikiwa ni kitovu cha elimu kwa wakulima, wafanyabiashara katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Cc @wizara_ya_kilimo







Tanzania, Indonesia kuendeleza ushirikiano katika sekta ya kilimo Tanzania, Indonesia kuendeleza ushirikiano katika sekta ya kilimo Reviewed by Zero Degree on 8/03/2025 01:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.