Loading...

Kisa Cocaine, Mrisho ahukumiwa kifungo cha maisha


Tarehe 23 Septemba 2025, Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Hemedi Juma Mrisho maarufu kama Horohoro, baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 31 Oktoba 2023, katika eneo la Boko Magengeni, mkoa wa Dar es Salaam, Maafisa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya walimkamata Hemedi Juma Mrisho akiwa na gari aina ya BMW X5 lenye namba za usajili T189 DWY, ambapo wakati wa upekuzi, walibaini dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa gramu 326.46 pamoja na silaha moja ya moto, bastola aina ya Fatih 13.

Baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alifikishwa mahakamani ambapo kesi yake iliendeshwa chini ya shauri la kiuchumi namba 34390/2025. Mashahidi mbalimbali waliwasilisha ushahidi, na mahakama iliridhika bila shaka kuwa mtuhumiwa alikuwa na hatia.

Hukumu hii inatajwa kuwa ni ujumbe kwa wote wanaojihusisha au kufikiria kujiingiza kwenye biashara ya dawa za kulevya kuwa sheria haitasita kuchukua mkondo wake.
Kisa Cocaine, Mrisho ahukumiwa kifungo cha maisha Kisa Cocaine, Mrisho ahukumiwa kifungo cha maisha Reviewed by Zero Degree on 9/23/2025 07:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.