Loading...

Baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar, Abdi Banda afungiwa mechi 2

Beki wa timu ya Simba SC Abdi Banda amekutana na adhabu ya kufungiwa michezo miwili na kamati ya haki na hadhi za wachezaji baada ya kukutwa na kosa la kumpiga mchezaji wa Kagera Sugar wakati wa mchezo dhidi ya Simba dhidi ya Kagera.

Banda alifanya kosa hilo wakati wa mchezo huo uliyochezwa April 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba kwa kumpiga ngumi George Kavilla wa Kagera Sugar lakini adhabu yake imepungua kutokana na Banda kuwa alimuomba radhi Kavilla lakini pia alikiri kosa.

Beki huyo wa Simba anayechipukia, jana aliingia kwenye kikao cha kamati hiyo na kuomba radhi.

Taarifa zinaeleza, Banda aliomba radhi mbele ya kikao baada ya kukiri kosa.

“Kingine kilichomsaidia Banda ni kwa kuwa alimuomba radhi mchezaji husika (Kavila) na mchezaji huyo akakiri kuombwa radhi na Banda,” kilieleza chanzo ndani ya kamati.

Sasa Banda ana nafasi ya kuendelea kuitumikia Simba katika michezo mitatu iliyosalia baada ya kumaliza kuitumikia adhabu hiyo, katika mchezo huo Simba ilifungwa na Kagera kwa magoli 2-1.

Source: SalehJembe
Baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar, Abdi Banda afungiwa mechi 2 Baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar, Abdi Banda afungiwa mechi 2 Reviewed by Zero Degree on 4/20/2017 03:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.