Familia yatengwa kisa ugonjwa wa ngozi mkoani Rukwa
Mtoto anayeugua ugonjwa wa ngozi |
Paroko wa Kanisa Katoliki, lililopo katika kata ya Kate, Padre Jofrey Kitaya ndiye aliyemwokota mtoto Peter Kazumba (13), aliyelala usiku kucha pembezoni mwa Zahanati ya Mtakatifu Anna, inayomilikiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki iliyopo katika kijiji cha Kate .
Mtoto Peter ambaye hasomi na hajawahi kuingia darasani, anasumbuliwa na ugonjwa sugu wa ngozi, ambao umemfanya aharibike na kutoa harufu kali, huku akiwa na jeraha kubwa la moto katika goti lake la mguu wa kushoto na anaonekana mzee kuliko umri wake.
Baba mzazi na majirani ambao wao katika mazungumzo yao, walihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Martin Kazumba (36) alidai kuwa amekuwa akimpeleka mtoto wake huyo katika Kituo cha Afya kilichopo katika kijiji jirani cha Mvimwa wilayani Nkasi, kwa matibabu kwa miaka mitano mfululizo bila mafanikio.
Wakati hayo yakijiri mama mzazi wa mtoto Peter pamoja na watoto wengine, walikuwa shambani mbali na kijiji hicho. Kwa upande wake, mtoto Peter alimwomba Rais John Magufuli na wasamaria wema, waguswe na ugonjwa alionao, ambao unampatia mateso makubwa, wamsaidie gharama za matibabu.
Kwa upande wake, Mganga wa Kituo cha Afya cha Kate, Abdallah alieleza kuwa ugonjwa huo kitatibu unajulikana kama Adematomycosis na kwamba mtoto huyo amepatwa na usugu wa ugonjwa huo wa ngozi, unaosababishwa na fangasi.

“Ilikuwa Jumatatu ya Pasaka asubuhi nilikuwa nimetoka kuongoza ibada ya Misa Takatifu, basi nikashuka hadi zahanati ndipo nilipomwona mtoto huyu akiwa amelala pembeni mwa ukuta wa zahanati.
Jinsi alivyoharibika mwili wake, nilidhani ama nimetokewa na Yesu Mfufuka katika sura ya mateso au Lazaro, sikuamini macho yangu nilipatwa na mshtuko mkubwa mno, kwani inahitaji imani ya ziada kuzungumza na mtoto huyo jinsi alivyo .
Nilimchukua hadi kwa watawa wa Kanisa Katoliki hapa Kate, wakampatia kinywaji baridi na keki kwa jinsi alivyokuwa anakula ni wazi alikuwa amebanwa na njaa na kiu,” alisema Padri Kitaya.
Baba mzazi na majirani ambao wao katika mazungumzo yao, walihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Martin Kazumba (36) alidai kuwa amekuwa akimpeleka mtoto wake huyo katika Kituo cha Afya kilichopo katika kijiji jirani cha Mvimwa wilayani Nkasi, kwa matibabu kwa miaka mitano mfululizo bila mafanikio.
“Tayari nimefilisika kwa ajili ya kugharamia matibabu ya mtoto wangu huyu, amekuwa akitibiwa kwa miaka mitano mfululizo bila kupona huku hali yake ikiendelea kuwa mbaya kila kukicha.
Isitoshe mke wangu, mimi mwenyewe na watoto wengine watano, akiwemo wa mwaka, tumeshaambukizwa ugonjwa huu. Nimekata tamaa sijui la kufanya hakika nimechoka inawezekana tumerogwa kwa nini ni sisi tu yaani hii familia yangu pekee ?” alihoji.
Wakati hayo yakijiri mama mzazi wa mtoto Peter pamoja na watoto wengine, walikuwa shambani mbali na kijiji hicho. Kwa upande wake, mtoto Peter alimwomba Rais John Magufuli na wasamaria wema, waguswe na ugonjwa alionao, ambao unampatia mateso makubwa, wamsaidie gharama za matibabu.
Akizungumza kwa taabu, alisema, “Sina raha kabisa kuendelea kuishi kwa kuwa hata majirani zetu wananitenga, watoto wenzangu pia hawako tayari kucheza wala kula na mimi”. Baadhi ya wakazi wa kata hiyo kwa nyakati tofauti, walikiri kuingiwa na hofu kubwa ya kuweza kuambukizwa ugonjwa huo, waliouita wa ajabu.
“Sio siri tunaogopa hata kwenda kumjulia hali jirani yetu tukihofia kuambukizwa ugonjwa huo. Kijiji kinaamini hauna tiba,” alieleza mkazi wa kijiji hicho, Ignas Kipeta. Akizungumza, Padri Kitaya alisema, “ Wapendwa Taifa la Mungu, sote tuguswe na madhira yaliyompata mtoto huyu (Peter) na familia yake , si kazi rahisi kwa mtu mmoja pekee bali Serikali, kanisa, taasisi mbalimbali na watu binafsi, tuguswe na kujitokeza kuisaidia familia hii ambayo imekubikwa na mateso makubwa ya kimwili na kiroho”.
Kwa upande wake, Mganga wa Kituo cha Afya cha Kate, Abdallah alieleza kuwa ugonjwa huo kitatibu unajulikana kama Adematomycosis na kwamba mtoto huyo amepatwa na usugu wa ugonjwa huo wa ngozi, unaosababishwa na fangasi.
“Ugonjwa huu ni hatari kwa sababu unaambukiza na unaweza kuenea kirahisi katika jamii nzima na kusambaa zaidi lakini licha ya kuwa ni hatari bado unatibika. Tatizo mtoto huyu hawezi kulazwa kwa matibabu katika zahanati na vituo vya afya kwani anahitaji uangalizi maalumu. Nashauri apelekwe katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa iliyoko katika Mji wa Sumbawanga, ambako kuna wataalamu, mtoto huyu anatakiwa awe chini ya uangalizi wa jopo la wataalamu wa afya,” alisema.
Source: Habari Leo
Familia yatengwa kisa ugonjwa wa ngozi mkoani Rukwa
Reviewed by Zero Degree
on
4/20/2017 04:10:00 PM
Rating: