Loading...

Zaidi ya walimu 20,000 kutoka Tanzania bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya

Picha ya Mtandao: Baadhi ya Walimu  wakifuatilia semina ya mafunzo kwa walimu jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa wa shule za msingi
Walimu 22,993 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya na uimarishaji wa ufundishaji wa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu kwa walimu wa somo la hisabati na lugha wa darasa la tatu na la nne, yanayoendeshwa na Wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu ( ADEM ) kwa kushirikiana na Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Mtendaji Mkuu wa ADEM Dk.Siston Masanja amesema mafunzo hayo ya mtaala ulioboreshwa kwa sasa yanawashirikisha takribani 9,060 katika mikoa 7 ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Mara, Shinyanga, Simiyu na Tabora na kuongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ubora wa elimu kwa kuwajengea uwezo na umahiri walimu katika kufundisha ili kutimiza adhima ya serikali ya kuondoa tatizo la wanafunzi kutomudu stadi za kkk.

Mratibu wa Mafunzo hayo Masumbuko kossey,amesema walimu 492 kutoka halmashauri tatu za wilaya ya itilima, Bariadi vijijini na Busega mkoani Simiyu ndio wanaohudhuria mafunzo hayo ya mtaala ulioboreshwa awamu ya pili, amewataka washiriki kujiepusha na vitendo vya utoro, ulevi na uzembe wakati wa mafunzo na kuwa mabalozi wa wenzao ambao wamebaki katika vituo vyao vya kazi ili kujenga uelewa wa pamoja na wenye ufanisi kielimu.

Matarajio ya walimu wote 1,032 wa shule 516 za msingi mkoani Simiyu,ambao wamehudhuria mafunzo hayo kwa awamu mbili kuanzia Aprili 6 hadi 23 mwaka huu yatapofungwa rasmi, ni kwenda kutoa maarifa thabiti yanayolenga kukuza stadi za maisha na ufaulu katika mitihani ya kitaifa ya elimu ya msingi pamoja na kuongeza ufanisi, utendaji na utekelezaji wa sera na mipango ya kielimu kitaifa, hususani sera ya elimu bure.
Zaidi ya walimu 20,000 kutoka Tanzania bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya Zaidi ya walimu 20,000 kutoka Tanzania bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya Reviewed by Zero Degree on 4/20/2017 03:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.