Loading...

Chelsea wamalizana na Monaco kwa Bakayoko, anatarajiwa kwa vipimo Ijumaa


Kwa mujibu wa habari zilizoripotiwa, Timoue Bakayoko anatarajiwa kufanya vipimo vya afya Ijumaa ijayo.

Chelsea wamepanga ratiba hiyo ya vipimo kwa Bakayoko baada tu ya Monaco kukubali dau la paundi milioni.

'The Blues' wamekuwa katika mapatano yaliyokuwa na mvutano mkubwa kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo kwa miezi kadhaa iliyopita, na hata kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Manchester United waliojitokeza mwishoni ambao hivi karibuni wamefanikiwa kutibua dili la Chelsea na Romelu Lukaku kwa mtindo huo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti za Kituo cha Redio cha RMC nchini Ufaransa, Chelsea wamefanikiwa kuwapiku mahasimu wao na kufanikisha kumnasa kiungo huyo, Timoue Bakayoko, ambaye atahamia Magharibi ya London kwa dau la paundi milioni 40.

Meneja huyo wa Kiitaliano (Conte) inasemekana bado anahitaji wachezaji wengine wapya watano kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Chelsea wamalizana na Monaco kwa Bakayoko, anatarajiwa kwa vipimo Ijumaa Chelsea wamalizana na Monaco kwa Bakayoko, anatarajiwa kwa vipimo Ijumaa Reviewed by Zero Degree on 7/13/2017 10:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.