Loading...

Orodha ya makocha walioshinda Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930


Kombe la Dunia ni mashindano ya soka ya kimataifa yanayojumuisha timu za kitaifa za wanaume, wanachama wa FIFA. Michuano hiyo hufanyika kila baada ya miaka minne tangu kuzinduliwa mwaka 1930, isipokuwa mwaka 1942 na 1946 ambapo michuano haikufanyika kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kwa mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka huu (2018) na mabingwa wa sasa ni Ufaransa.

Tangu mwaka 1930, mashindano ya Kombe la Dunia yameshafanyika mara 20 na timu nane tofauti zimeshafanikiwa kushinda mashindano hayo. Brazil wakiwa vinara, baada ya kutwaa mataji matano. Brazili inajulikana sana kwa kucheza mpira wa kuvutia maarafu kama 'Joga Bonito'. Ujerumani na Italia zinafuata baada ya kushinda vikombe vinne kila mmoja. Uruguay na Argentina ni kati ya mataifa pekee yaliyofanikiwa kushinda kombe hilo zaidi ya mara moja, ambapo kila mmoja ameshatwaa taji hilo mara mbili. Uingereza, Ufaransa na Hispania wote wameshinda kombe la dunia mara moja kila mmoja.

Ufaransa, ambayo inanolewa na Didier Dechamps ilishinda Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kumpiga Ubelgiji na kutinga fainali kisha ikaitandika Croatia kichapo cha mabao 4-2.

Inayofuata hapo chini ni orodha ya makocha walioshinda kombe la dunia:
  • Alberto Suppici, Uruguay (Kombe la Dunia mwaka 1930)
  • Vittorio Pozzo, Italy (Kombe la Dunia mwaka 1934 na 1938)
  • Juan López, Uruguay (Kombe la Dunia mwaka 1950)
  • Sepp Herberger, Ujerumani magharibi (Kombe la Dunia mwaka 1954)
  • Vicente Feola, Brazil (Kombe la Dunia mwaka 1958)
  • Aymoré Moreira, Brazil (Kombe la Dunia mwaka1962)
  • Alf Ramsey, Uingereza (Kombe la Dunia mwaka 1966)
  • Mário Zagallo, Brazil (Kombe la Dunia mwaka 1970)
  • Helmut Schön, Ujerumani magharibi (Kombe la Dunia mwaka 1974)
  • César Luis Menotti, Argentina (Kombe la Dunia mwaka 1978)
  • Enzo Bearzot, Italia (Kombe la Dunia mwaka 1982)
  • Carlos Bilardo, Argentina (Kombe la Dunia mwaka 1986)
  • Franz Beckenbauer, Ujerumani magharibi (Kombe la Dunia mwaka 1990)
  • Carlos Alberto Parreira, Brazil (Kombe la Dunia mwaka 1994)
  • Aimé Jacqueti, Ufaransa (Kombe la Dunia mwaka 1998)
  • Luiz Felipe Scolari, Brazil (Kombe la Dunia mwaka 2002)
  • Marcello Lippi, Italia (Kombe la Dunia mwaka 2006)
  • Vicente del Bosque, Hispania (Kombe la Dunia mwaka 2010)
  • Joachim Löw, Ujerumani (Kombe la Dunia mwaka 2014)
  • Didier Deschamps, Ufaransa (Kombe la Dunia mwaka 2018)
Orodha ya makocha walioshinda Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930 Orodha ya makocha walioshinda Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930 Reviewed by Zero Degree on 10/20/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.