Loading...

Pires: Arsenal itamaliza Ligi Kuu katika nafasi hii msimu huu


Aliyekuwa nyota wa klabu ya Arsenal, Robert Pires anaamini kwamba klabu hiyo itamaliza ligi katika nne za juu chini ya Unai Emery msimu huu. Gunners walianza vibaya mwanzoni mwa msimu kwa kupoteza michezo dhidi ya Manchester City na Chelsea. Hata hivyo, wamerudi na nguvu na wameshinda mechi 9 mfululizo. Arsenal sasa iko nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi, pointi mbili tu nyuma ya Manchester City, Chelsea na Liverpool.

Emery anastahili kusifiwa kwa mabadiliko aliyoiletea Arsenal baada ya kuchukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa miaka 22.

Arsenal ilimaliza misimu miwili iliyopita katika nafasi ya 6 na 5 kwa mtiririko huo. Hata hivyo, Pires anaamini Emery anaweza kuirejesha klabu hiyo katika nafasi nne bora msimu huu.

Robert Pires
Pires alisema, "Kwa sasa ninaifurahia sana klabu kwa sababu mimi ni balozi wa Arsenal lakini hasa kwa Unai Emery kwa sababu yeye ni meneja mkubwa. Alifanya vizuri na Sevilla, alishinda mataji kadhaa, hasa na Paris Saint-Germain msimu uliopita. Na bila shaka unajua unahitaji kufanya maboresho kila siku lakini kusema kweli Arsenal iko vizuri, hasa katika Ligi Kuu.

Michezo tisa, ushindi mara tisa hivyo nadhani watamaliza katika nne za juu, ni uhakika asilimia 100. "

Tangu kushindwa kwao dhidi ya Chelsea, Arsenal haijakabiliwa na timu yoyote kubwa. Mechi yao ijayo dhidi ya timu kubwa ni dhidi ya Liverpool tarehe 3 Novemba. Leo Jumatatu usiku washika bunduki hao wataikabili Leicester City.
Pires: Arsenal itamaliza Ligi Kuu katika nafasi hii msimu huu Pires: Arsenal itamaliza Ligi Kuu katika nafasi hii msimu huu Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.