Hatimaye Simba SC yapata kocha msaidizi
Nafasi hiyo iliyoachwa wazi mwanzo mwa msimu huu na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma, imezibwa na kocha mtanzania Denis Kitambi.
Kitambi amewahi kuzifundisha vilabu vya Ndanda FC akiwa kama kocha mkuu, Azam FC akiwa kocha msaidizi chini ya Stewart Hall ambaye pia alikwenda kufanya naye kazi kama kocha wake msaidizi katika klabu ya AFC Leopards ya Kenya.
Msemaji wa Simba Haji Manara ameeleza moja ya malengo makuu ya kumpa nafasi kocha huyo kijana na kuhakikisha anaisaidia klabu katika kutetea ubingwa wa ligi kuu pamoja na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kitambi ambaye tayari amekwishajiunga na kambi ya timu hiyo jijini Dar es Salaam, ajana ametambulishwa rasmi kwa umma na mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi utakuwa ni dhidi ya Yanga unaopigwa leoi kwenye uwanja wa taifa.
Hatimaye Simba SC yapata kocha msaidizi
Reviewed by Zero Degree
on
2/16/2019 07:35:00 AM
Rating: