Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Februari 14, 2019
Manchester United wanatarajiwa kutangaza dau la usajili kwa winga wa Benfica Joao Felix, 19, mwishoni mwa msimu.
Juventus wamegoma kumuuza mshambuliaji wao raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, mwishoni mwa msimu. Hilo ni Pigo kwa Manchester United na Chelsea ambao walikuwa wanamnyemelea.
Manchester City wataminyana na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa Lyon, Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, mwishoni mwa msimu. (Sun)
Manchester United wamewekeza nguvu zao kuwasajili wachezaji wanne mwishoni mwa msimu ambao ni: Kalidou Koulibaly, 27, kutoka Napoli, Lucas Hernandez, 22, wa Atletico Madrid, Nikola Milenkovic, 21, wa Fiorentina na Douglas Costa, 28, wa Juventus. (Mirror)
Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany anatarajiwa kukubali kukatwa mshahara ili kusaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi na klabu hiyo. Mlinzi huyo raia wa Ubelgiji, 32, anatarajiwa kuandaliwa mchezo wa kumbukumbu mwezi Agosti mwaka huu. (Mail)
Kocha wa Leicester Claude Puel amesema kupokea ofa kutoka kwa Manchester City, Manchester United na Tottenham ili kuwasajili wachezaji Ben Chilwell, Harry Maguire na James Maddison mtawalia kunaonesha namna gani klabu yake inavyofanya kazi nzuri ya kukuza vipaji. (Leicester Mercury)
Timo Werner, 22 |
Wachezaji wa Liverpool Naby Keita na Sadio Mane wamemshawishi straika wa Ujerumani Timo Werner, 22, kuhamia Anfield iwapo ataondoka RB Leipzig mwishoni wa msimu. (ESPN)
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ametangaza kuwa mshambuliaji raia wa Argentina Lionel Messi, 31, anatarajiwa kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2021. (RKB, kupitia Marca)
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri yupo kwenye shinikizo kubwa la kushinda taji la Europa ili kulinda kibarua chake. (Telegraph)
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri yupo kwenye shinikizo kubwa la kushinda taji la Europa ili kulinda kibarua chake. (Telegraph)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Februari 14, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
2/14/2019 08:05:00 AM
Rating: