Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 15, 2019


Juventus itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Tuttosport)

Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Celtic na mlinzi wa Scotland Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 21. Leicester inamtaka Tierney aichukue nafasi ya mlinzi Ben Chilwell wakati wakitarajia maombi kuwasilishwa kwa mchezaji huyo. (Mirror)

Gunners imefanya mazungumzo na winga wa zaidi ya miaka 21 wa Rennes Ismaila Sarr. Arsenal imeipiku klabu hiyo ya Ufaransa kufika katika robo fainali ya Ligi ya Uropa Alhamisi. (Goal France)
Lawrence Masira: Mvulana wa Kenya aliyetunukiwa na mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil

Manchester United wamejiunga katika kutaka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa PSG Adrien Rabiot, wa miaka 23. Raia huyo wa Ufaransa hana mkataba ifikapo msimu wa joto na tayari amezungumza na Barcelona, Arsenal, Chelsea na Tottenham.

Burnley inatazamia kumuuza Nick Pope, wa miaka 26, kwa kiasi cha £10m msimu huu wa joto, huku Arsenal ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili kipa huyo wa England. (Sun)

PSG itamkabidhi meneja Thomas Tuchel mkataba wa mwaka mmoja zaida. Raia huyo wa Ujerumani alisaini mkataba wa miaka miwili mnamo Mei 2018.

Newcastle ina hamu ya kumuajiri meneja wa Lyon Bruno Genesio iwapo Rafael Benitez hatoongeza mkataba wake huko St James' Park. (L'Equipe)

Meneja wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane anataka kumsajili kiungo cha mbele wa Ufaransa na Lyon Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 25, katika msimu wa joto. (Daily Record)
Timu hiyo kuu ya Uhispania huenda ikatoa sehemu ya fedha hizo katika kumsajili mchezaji wa miaka 19 wa kiungo cha kati wa timu ya Roma Nicolo Zaniolo.

Lakini Zidane hana hamu ya kumchukua mchezaji wa kiungo cha mbele wa PSG Neymar, wa miaka 27, kwenda Bernabeu. (AS)

Eder Militao
Baada ya kumsajili mchezaji wa Brazil na Porto Eder Militao, Tayari Real imefikia kiwango cha mwisho kinachotakiwa cha wachezaji wasio raia wa Umoja wa Ulaya kwa mwaka ujao, na kufanya kuwa na uwezekano mkubwa kwa mchezaji wa Colombia, James Rodriguez kutojiunga nao punde tu mkataba wake wa miaka miwili utakapomalizika huko Bayern Munich. (Marca)

Real inataka kukusanya £128m katika mauzo ya wachezaji msimu huu wa joto na itaomba £42.7m kwa wachezaji Rodriguez na mchezaji wa kiungo cha kati wa Croatia Mateo Kovacic, kila mmoja, ambaye kwa sasa yuko Chelsea kwa mkopo. (El Confidencial)

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Fulham Slavisa Jokanovic na bosi wa Preston Alex Neil ndio wanaopigiwa upatu kuijaza nafasi ya meneja wa timu ya West Brom. (Sky Sports)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 15, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 15, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/15/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.