Daktari Mfaransa atuhumiwa kwa kuwapa sumu wagonjwa 24
Daktari mmoja Mfaransa ambaye tayari anachunguzwa kwa kuwapa sumu wagonjwa saba ameshitakiwa kwa kuwapa sumu watu wengine 17 katika kliniki moja ya mashariki mwa Ufaransa.
Frederic Pechier, mwenye umri wa miaka 47, sasa anakabiliwa na mashitaka 24, ambapo matukio tisa yalisababisha vifo, baada ya kufanya kazi kama daktari bingwa katika kliniki mbili za kibinafsi kwenye mji wa mashariki mwa Ufaransa wa Besancon.
Kama atapatikana na hatia, Pechier huenda akahukumiwa kifungo cha maisha. Wakili wake amesema leo kuwa Pechier aliachiliwa huru bila masharti usiku wa kuamkia leo. Mwendesha mashitaka Etienne Manteaux alikuwa anataka daktari huyo kuwekwa kizuizini.
Pechier ambaye alishitakiwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 kwa vifo viwili katika kesi saba za kupewa wagonjwa sumu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, alihojiwa wiki hii kuhusiana na matukio 66 yalioshukiwa kuwa ya mshtuko wa moyo wakati akiwafanyia upasuaji wagonjwa ambao hawakuonekana kuwa katika hatari kubwa.
Daktari Mfaransa atuhumiwa kwa kuwapa sumu wagonjwa 24
Reviewed by Zero Degree
on
5/18/2019 08:20:00 AM
Rating: