Loading...

Dar es salaam kinara watu wenye ugonjwa wa Dengue


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi amesema wagonjwa 1,901 wamebainika kuwa na virusi vya Dengue Tanzania, huku wengine wakiwa tayari wamepona na baadhi wengine wakiwa wanapata tiba.


Prof. Kambi ametoa ripoti hiyo leo Jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa Dar es salaam ni Mkoa pekee unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi 1809 Tanzania nzima.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa mpaka sasa dawa inayosaidia kupunguza makali ya ugonjwa huo ni Panadol na kunywa maji safi na salama, sambamba na kukaa katika mazingira yasiyozalisha mbu aina ya AIDES.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dk. Yudas Ndungile, amesema wilaya zote zimeathirika na ugonjwa wa Dengue huku Ilala ikiwa na wagonjwa 235
Dar es salaam kinara watu wenye ugonjwa wa Dengue Dar es salaam kinara watu wenye ugonjwa wa Dengue Reviewed by Zero Degree on 5/16/2019 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.