Mbunge aeleza sababu za kuangua kilio bungeni
Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema), ameeleza sababu za kuangua kilio bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kuwa ni kutokana na adha ya ubovu uliokithiri wa barabara ya Mlimba hadi mpakani mwa Mkoa wa Njombe eneo la Lwamote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mtanzania, Kiwanga amesema hali katika barabara hiyo ni mbaya na katika kipindi hiki cha mvua mabasi ya abiria yanayojaribu kwenda kule yanakaa njiani zaidi ya siku tatu huku abiria wengine wakiwa ni wagonjwa, watoto na wazee.
“Hivi ninavyoongea hata kijiko kilichokwenda kukwamua magari yaliyokwama na kusawazisha baadhi ya maeneo kwenye barabara hiyo kimezama kabisa, kuna basi lilikwama kwa siku tatu, wananchi wanataabika, nilipokumbuka adha hizo nilijikuta ninatoa machozi.
“Kuna hatari watu wengine wanaweza kupata magonjwa ya mshtuko kama presha na hata kufia njiani kwa sababu kama kijiko (katapila) kinazama unategemea nini kwa mabasi ya kawaida?,” alihoji Kiwanga.
Mbunge aeleza sababu za kuangua kilio bungeni
Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2019 10:50:00 AM
Rating: