Loading...

Mbunge aitaka serikali kuhalalisha bangi


Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba anataka serikali kuhalalisha matumizi ya bangi ama marijuana nchini tanzania kwa mautumizi ya dawa.

Aliambia bunge siku ya Jumatatu kwamba mataifa mengine manne ya Afrika tayari yemahalalisha Marijuana kutumiwa kutengeneza dawa.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania mbunge huyo anasema kuwa ni vyema kama taifa kuanza kufikiria kuhusu fursa hiyo mapema.

''Tunavyozungumza, Uganda imehalalaisha upanzi wa Marijuana kwa matumizi ya dawa'', alisema akitaja ripoti za hivi majuzi kwamba taifa hilo la Afrika mashariki limenunua mbegu kupanda mmea huo.

''Sijui ni kwa nini kitengo cha chakula na dawa hakijachukua sampuli kuelezea serikali kwamba dawa hizo zina bangi ndani yake'', alihoji.

Kulingana na gazeti hilo ,bangi kama inavyojulikana ni haramu nchini Tanzania na inavutia hukumu kali jela na faini kubwa.

''Tuna bangi lakini kile kinachoonekana kila siku ni maafisa wa usalama kuharibu mmea huo. Bangi imetumika kwa miaka kadhaa kutengeneza dawa''.
Bangi hutumika kutengeneza dawa

Alisema kwamba Lesotho na Zimbabwe zilihalalisha utumizi wake akiongezea kwamba amewahi kuona kiwanda kinachotengeneza dawa kwa kutumia bangi.

Aliongezea kuwa gunia moja la bangi linauzwa kati ya Sh4 million na Sh4.5 millioni huku likiuzwa Sh20 millioni nchini Zimbabwe na Lesotho.

WebMD, Mtandao unaotoa habari za kiafya unasema kuwa ushahidi mkubwa kuhusu mmea wa bangi ni uwezo wake wa kupunguza maumivu, kichefuchefu na kutapika baada ya mgonjwa kupatiwa tiba ya kutumia kemikali {chemotherapy}.

Kulingana na The Citizen Tanzania Uganda inatarajiwa kuuza bangi inayotumika kama dawa yenye thamani ya Shilingi bilioni 600 billion mwezi Juni kwa taifa la Canada na Ujerumani ikilinukuu gazeti la The Daily Monitor nchini Uganda.
Imani ya Rastafari

Imebainika kwamba mnamo tarehe 7 mwezi Disemba Uganda iliuza bangi, na mauwa yenye thamani ya $10,000 kwa kampuni moja ya Afrika kusini.

Muungano wa Rastafari nchini Tanzania ni mojawapo wa mashirika ambayo yanashinikiza wazo la kuhalalishwa kwa bangi katika taifa hilo.



Rasta wanaamini kwamba mmea wa 'Tree of Life' uliotajwa katika bibilia ni ule wa bangi.

Mbali na imani za wengi , Rasta hushutumu matumizi ya marijuana kwa lengo la ulevi.

Wale wanaounga mkono wazo la mmea huo kuhalalishwa nchini Tanzania ni pamoja na mbunge wa Geita mashambani muheshimiwa Joseph Msukuma.

Katika kikao cha bunge Msukuma alisema kuwa hajawahi kusikia ama kuona utafiti wowote wa kisayansi uliopata bangi na miraa kuwa na tatizo lolote.

Alisema kuwa hatua ya serikali kuharamisha mimea hiyo haina msingi wowote.
Msimamo wa Serikali.

Hatahivyo serikali ya Tanzania imepinga uwezekano wowote wa kuhalalishwa kwa mmea huo katika taifa hilo.

Mnamo mwezi Februari 2016, naibu waziri wa afya Dkt. Hamis Kigwangalla alipinga kuhalalishwa kwa bangi na miraa ahihusisha utumizi wake na matatizo ya kiakili .

''Tafiti kadhaa zimethibitisha kwamba matumizi ya marijuana yanasababisha matatizo ya kiakili na hivyobasi serikali haiwezi kuhalalisha matumizi yake'', alisisitiza Kigwangalla.

Lakini mwenyekiti wa Rastafari United Front Thau-Thau Haramamba anasema kuwa matatizo ya kiakili yanayowakabili watumizi wa bangi hayatokani na matumizi ya bangi badala yake uchanganyaji wa bangi na vitu vileo vingine.

Anahoji kwamba hakuna utafiti umewahi kupata matumizi ya mmea huo kushirikishwa na tatizo la Kiakili.

Chanzo: BBC
Mbunge aitaka serikali kuhalalisha bangi Mbunge aitaka serikali kuhalalisha bangi Reviewed by Zero Degree on 5/21/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.