Loading...

Waziri atoa onyo utekelezaji katazo la mifuko

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba, amesema utekelezaji wa agizo la kuzuia mifuko ya plastiki halitakuwa la kunyanyasa wananchi kwa kuwapora mali zao na kuleta usumbufu kwa namna moja ama nyingine.

January Makamba ametoa angalizo hilo leo kwenye kikao cha viongozi na watendaji wa Mkoa wa Dar es salaam katika majadiliano ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki na nakuongeza kuwa zoezi hilo lisitumike kama fursa ya kuwanyanyasa wananchi, ambao baadhi yao kuna uwezekano hawajafikiwa na elimu hiyo vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara amezitaka mamlaka hizo kutenga maeneo maalum yakuhifadhi mifuko hiyo na kubadilishaa matumizi yake ili isiwe sumu kwenye mazingira wakati zoezi la katazo likindelea.

Faini kwa watengenezaji ni Milioni 20 hadi Bilioni 1 na kifungo cha miaka 2, wakati wasafirishaji faini ni Milioni 5 mpaka Milioni 20 na kifungo cha miaka 2, kwa upande wa wauzaji wa rejareja faini laki 1 mpaka laki 5 na kifungo cha miezi 3 na kwa wale wanaoibeba faini elfu 30 mpaka laki 2 na kifungo cha siku 7.
Waziri atoa onyo utekelezaji katazo la mifuko Waziri atoa onyo utekelezaji katazo la mifuko Reviewed by Zero Degree on 5/21/2019 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.