Loading...

Abiy Ahmed: Hakuna cha kutuzuia kujenga bwawa mto Nile


Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema kuwa hakuna kitu chochote kitakachoweza kuizuia Ethiopia kujenga bwawa kwenye mto Nile.

Waziri Abiy ambaye pia ni mshindi wa Tuzo la Amani ya Nobel atoa kauli hiyo kufuatia pingamizi kutoka Misri juu ya mnradi huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, bwawa hilo linalotarajiwa kujengwa katika Mto Nile Kaskazini mwa Ethiopia, litaunda kituo kikuu cha umeme barani Afrika. 

Inaelezwa kuwa karibu asilimia 85 ya Mto Nile hutoka katika nyanda za juu za Ethiopia.

Hata hivyo, Serikali ya Misri inaogopa mradi huo kwa madai kuwa utaruhusu kudhibiti mtiririko wa maji katika mto huo.

Kutokana na tamko hilo, nchi hizo zimejikuta katika mgogoro na mvutano wa kisiasa kwa muda mrefu.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa kufuatia mgogoro huo, Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Ethiopia mapema leo asubuhi Oktoba 23 wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi-Afrika unaofanyika nchini Urusi.

Rais Sisi pia anatarajiwa kupendekeza kuteuliwa kwa mpatanishi ili kusuluhisha mzozo huo wa muda mrefu huku kiongozi huyo wa Ethiopia akisema kuwa anataka kusisitiza ukweli kwamba hakuna nguvu inayoweza kuzuia kukamilika kwa bwawa hilo.

"Watu wa Ethiopia hawana nia ya kuwadhuru watu wa Misiri, wanahitaji tu kufaidika na bwawa,” alisisitiza Rais Abiy alipokuwa akizungumza na wabunge katika mji wa Addis Ababa.

Ethiopia inatarajia kuwa bwawa hilo ambalo inaelezwa kuwa ni kubwa zaidi litakalokamilika ifikapo mwaka 2021. Kwa sasa Misiri inatumia zaidi maji ya mto huo na ripoti za Umoja wa Mataifa (UN), zinatabiri kuwa nchi hiyo yenye karibu watu milioni 100, itaanza kupata shida ya uhaba wa maji ifikapo mwaka 2025.
Abiy Ahmed: Hakuna cha kutuzuia kujenga bwawa mto Nile Abiy Ahmed: Hakuna cha kutuzuia kujenga bwawa mto Nile Reviewed by Zero Degree on 10/23/2019 08:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.