UEFA: Samatta akili yote kwa Van Dijk leo
Leo Jumatano Samatta anatarajia kuiongoza Genk ya nchini Ubelgiji kucheza dhidi ya Liverpool katika mchezo wa tatu wa Kundi E linaloongozwa na Napoli yenye pointi 4, ikifuatiwa na Liverpool na Red Bull Salzburg ambao wote wana pointi tatu huku Genk ikiwa mkiani na pointi moja.
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Championi, baba mzazi wa mshambuliaji, mzee Ally Samatta alisema kuwa mtoto wake amejipanga kufanya vizuri katika mchezo huo ili kurahisisha ndoto yake ya kwenda kucheza ligi ya Uingereza.
“Binafsi nimeongea naye, amenihakikishia atafanya makubwa katika mchezo wao na Liverpool ambao utapigwa kesho (leo), Jumatano pale Genk kwa sababu mwenyewe akili yake yote ipo kwa yule beki bora wa dunia, Virgil van Dijk.
“Unajua hata mimi nimemueleza kwamba anatakiwa apambane haswa ikiwezekana yeye ndiyo acheze vizuri kuliko washambuliaji wote na amenihakikishia anamuonyesha van Dijk ubora wake kwa kuwa alishindwa kufanya hivyo kwa Kalidou Koulibaly wa Napoli kutokana na kumfahamu wakati wa Afcon kule Misri,” alisema mzee Samatta.
UEFA: Samatta akili yote kwa Van Dijk leo
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 08:20:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 08:20:00 AM
Rating:
