Loading...

Bondia Mtanzania achapwa raundi ya kwanza nchini Urusi


Bondia namba moja uzito wa juu Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo amepigwa na Mrusi, Arstan Yellev kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Urusi usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 6, 2019.

Katika pambano hilo la raundi 8, Mchumiatumbo alipigwa TKO kunako raundi ya kwanza, Ambapo bondia Arslan Yallyev alimsokomezea masumbwi mawili mazito yaliyompeleka chini Mchumitumbo mara mbili na kujikuta akisalimu amri.

Kocha Mtanzania aliyeambatana na bondia huyo, Anthony Rutha amesema refa alilazimika kumaliza pambano baada ya Mtanzania huyo kupelekwa chini mara mbili mfululizo.
Bondia Mtanzania achapwa raundi ya kwanza nchini Urusi Bondia Mtanzania achapwa raundi ya kwanza nchini Urusi Reviewed by Zero Degree on 10/06/2019 05:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.