Loading...

Jaji ajipiga risasi Mahakamani


JAJI Kanakorn Pianchana wa Thailand amejipiga risasi kifuani katika chumba cha mahakama baada ya kuwaachia huru watuhumiwa watano wa mauaji. Alitaka kujiua alipomaliza hotuba yake akishinikiza uwepo wa mfumo huru na wazi wa kimahakama kumtia mtu hatiani. Sasa anapatiwa matibabu.

Wachambuzi wa mambo wanasema mahakama za Thailand kila mara kuwapendelea matajiri na wenye madaraka, lakini huwa zinatoa hukumu za haraka na ngumu kwa watu wa kawaida kwa makosa madogo jambo ambalo majaji huwa hawalilalamikii.


Jaji huyo alikuwa amewaachia Waislam watano waliokuwa wakituhumiwa kwa kuua kutumia bunduki Ijumaa iliyopita ambapo baada ya kufanya hivyo alitoa bastola na kujipinga kifuani.

“Unatakiwa kuwa na ushahidi wa wazi na wenye kuaminika ili kumwadhibu mtu. Hivyo, kama huna uhakika, usimwadhibu,” alisema jaji huyo kortini hapo.
Jaji ajipiga risasi Mahakamani Jaji ajipiga risasi Mahakamani Reviewed by Zero Degree on 10/07/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.