Kagere awainua mashabiki Taifa, Simba ikiilaza Azam kwa bao 1-0
Mchezo wa leo ambao umechezwa uwanja wa Taifa ulikuwa na ushindani mkubwa na ulitawaliwa na ubabe mwingi kutokana na kila timu kuhitaji kupata pointi tatu.
Simba wakiwa wenyeji wa mchezo iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 49 kuandika bao la kuongoza lililopachikwa kimiani na Kagere akimalizia pasi ya Francis Kahata kwa kichwa.
Ushindi huo unaifanya Simba kuzidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 15 na imecheza michezo mitano kwa kusepa na pointi zote tatu.
Beki wa Simba, Pascal Wawa ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwani aliokoa hatari nyingi kutoka kwa Chirwa ambaye alikuwa msubufu langoni akihaha kupata goli la ushindi ila bahati haikuwa yao.
Simba ilifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Sharaf Shiboub nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama, Hassan Dilunga alimpisha Miraj Athuman, Francis Kahata alimpisha Ibrahim Ajib kwa upande wa Azam FC alitoka Richard Djoud aliyempisha Chilunda, Frank Domayo alimpisha Donald Ngoma.
Kagere awainua mashabiki Taifa, Simba ikiilaza Azam kwa bao 1-0
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 06:50:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 06:50:00 PM
Rating:
