Loading...

Mbappe avunja rekodi ya Lionel Messi Ligi ya Mabingwa


Nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa aliteka hisa za mashabiki usiku wa jana Jumanne akitokea benchi na kuvunja rekodi ya kipekee.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe amevunja rekodi ya Lionel Messi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga magoli 15 kwenye Ligi ya Mabingwa.

Akiwa ametoka majeruhi katika siku za hivi karibuni, nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 aliingia uwanja katika kipindi cha pili cha mchezo PSG ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-0 ugenini dhidi ya Club Brugge na kuonyesha kuwa na faida dimbani kwa kutupia hat-trick.


Akiingia katika dakika ya 52, Mbappe alipachika bao lake la kwanza dakika ya tisa baada ya kuingia dimbani na kuongeza 'assist' muda mfupi akimsaidia Mauro Icardi.

Katika dakika ya 80, Mfaransa huyo alitupia bao la pili baada ya kufanikiwa kuwapita walinzi wawili na alikamilisha hat-trick dakika nne zilizofuata baada ya hapo kwa pasi iliyotoka kwa Angel Di Maria.

Hadi baada ya mchezo huo Mbappe anakuwa na mabao 15 ya Ligi ya Mabingwa katika umri wa miaka 20 na siku 306.

Rekodi hiyo inamfanya nyota huyo kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kupachika mabao mengi katika ligi hiyo maarufu Ulimwenguni na kufanikiwa kuvunja rekodi ya iliyokuwa ikishikiliwa na Messi, ambaye aliifikia rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 21 na siku 288.

Messi mwenye aliivunja rekodi ya nyota wa zamani wa klabu ya Real Madrid Raul aliyeandika rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 22 na siku 163, kitu amacho kinaifanya rekodi ya Mbappe kuwa ya kuvutia zaidi.

Hat-trick ya nyota huyo wa PSG pia inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu akitokea benchi tangu Joseba Llorente alivyofanya hivyo hivyo akiwa na Villarreal mwezi Oktoba 2008 dhidi ya Aalborg.
Mbappe avunja rekodi ya Lionel Messi Ligi ya Mabingwa Mbappe avunja rekodi ya Lionel Messi Ligi ya Mabingwa Reviewed by Zero Degree on 10/23/2019 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.