Loading...

Ngorongoro Heroes yatwaa ubingwa Cecafa U20, Kelvin John atikisa Afrika Mashariki


Ngorongoro Heroes leo Oktoba 10, 2019 imetwaa taji la CECAFA chini ya miaka 20 kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya.

Bao hilo pekee limepatikana mnamo dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kwa Otieno Onyango kujifunga.

Ushindi huo unaipa rasmi Tanzania kikombe hicho ambacho mashindano yake yalikuwa yanafanyika nchini Uganda.

Baada ya ushindi huo, Ngorongoro wanatarajia kurejea nchini kuanzia kesho.

Kelvin John ameibuka mchezaji bora wa mashindano hayo

Mshambuliaji Kelvin John wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, ameibuka mchezaji bora wa mashindano na mfungaji bora, akiwa amefunga goli 7 kwenye mashindano ya CECAFA U20.

Akizungumza baada ya mchezo wa fainali ambapo Tanzania U20 imeifunga Kenya U20 goli 1-0, Kelvin amesema kocha Zuberi Katwila alilkuwa anawaanda vizuri kwenye kila mechi.

Aidha Kelvina ameweka wazi kuwa anampenda nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kwasababu amefanikiwa na yeye anatamani kuwa kama yeye.
Ngorongoro Heroes yatwaa ubingwa Cecafa U20, Kelvin John atikisa Afrika Mashariki Ngorongoro Heroes yatwaa ubingwa Cecafa U20, Kelvin John atikisa Afrika Mashariki Reviewed by Zero Degree on 10/05/2019 06:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.