Loading...

Nitaipenda Arsenal daima - Arsene Wenger


Katika matukio ya hapa na pale ya kusisimua, shujaa wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alisema kwamba ataendelea kuipenda klabu hiyo siku zote.

Wenger anatimiza miaka 70 leo na ni meneja pekee katika Ligi Kuu ya Uingereza kumaliza msimu mzima bila kufungwa na pia kutwaa taji mbele ya mahasimu wake wakubwa wawili wa; Old Trafford na White Hart Lane Manchester United na Tottenham Hotspur.

Hivi karibuni katika mahojiano na mwandishi wa habari alisema kwamba haijalishi ataelekea wapi baada ya kutoka katika klabu hiyo, ataendelea kuipenda Arsenal.

Wakati alipokuwa bado ni meneja, Wenger alisema: “Ningependelea kukaa UK. Katika kazi ambayo nitaifanya siku zijazo, sijui kama nitakuwa huru siku ambazo Arsenal inacheza? Lakini nitafurahia kuwa UK kama nitapata tiketi.

“Kikubwa ni kwamba na mimi nitaweza kupiga kelele mbele ya meneja ajaye!”

Wenger amekua nje ya kibarua tangu ajiuzulu kutoka Arsenal mwezi Mei 2018. Wakati mashabiki walipoonekana kuchoshwa sana na mbinu za Wenger, pia wanamsifu kwa kuifikisha Arsenal mahili iliko leo hii kisoka na uimara wa kiuchumi.
Nitaipenda Arsenal daima - Arsene Wenger Nitaipenda Arsenal daima - Arsene Wenger Reviewed by Zero Degree on 10/23/2019 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.