Loading...

Sihitaji baunsa kwa sababu mashabiki mtaani wananilinda - Mr Blue


MSANII wa Hip Hop, Kherry Sameer ‘Mr Blue’ amesema yeye ni miongoni mwa wasanii ambao hawawezi kutumia walinzi binafsi ‘mabaunsa’, kwa ajili ya kumlinda kwenye maonesho wanayofanya.

Akizungumza jana Mr Blue amesema mashabiki zake ndiyo wanaomlinda hivyo hana sababu ya kutembea na mabaunsa.

“Sihitaji baunsa kwa sababu mashabiki mtaani wananilinda na sioni sababu ya mimi kulindwa, kwanza sina chuki na mtu, washikaji wengi wananipenda ila sisemi vibaya kwa wasanii wanaolindwa ili wawe salama, labda inawapa biashara kwenye maisha yao,” amesema Mr Blue.

“Pia kuwa au kutokuwa na ulinzi sio hoja ya msingi ila unangalia unawatumiaje hao walinzi kama kuwadhalilisha au kwa ajili ya kukulinda,” aliongeza Mr Blue.

Pia alisema kama wasanii wana ulinzi ikumbukwe hata wanasiasa pia nao ni watu ambao wana akili timamu na wamesoma, ila anashangaa hata dada wa uchochoroni, wauza vitumbua na magazeti nao wana ulinzi.
Sihitaji baunsa kwa sababu mashabiki mtaani wananilinda - Mr Blue Sihitaji baunsa kwa sababu mashabiki mtaani wananilinda - Mr Blue Reviewed by Zero Degree on 10/07/2019 02:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.