Loading...

Spurs yahofia kumpoteza Harry Kane


Tottenham Hotspur wanahofu kumkosesha raha Harry Kane kiasi cha kuhofia kumshuhudia akiondoka klabuni hapo Januari hii.

Spurs waliambulia kichapo cha mabao 7-2 katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Bayern Munich usiku wa Jumanne.

Mauricio Pochettino amekiri kuwa na mwanzo mgumu katika michuano ya msimu huu na kueleza ni jinsi gani hali inaweza kuwa ngumu zaidi. Kwa sasa Tottenham iko katika nafasi ya sita (6) kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupoteza michezo miwili kati ya saba hadi hivi sasa, mmoja ukiwa dhidi ya Newcastle United.

Kane anaelekea kutimiza miaka 27 mwezi wa Julai na bado hajashinda taji lolote katika muda wote ambao amekuwa na klabu hiyo. Tottenham bado haijatwaa taji lolote tangu kuwasili kwa Pochettino mwaka 2014 na si hapo, bali tangu mwaka 2008. Ushiriki wao wa fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliopita uliwaamsha wengi lakini mwamko huo ulififia muda mchache baaada ya majira ya joto.

Kane anachukuliwa kama mmoja wa washambuliaji bora katika EPL na Rio Ferdinand amemshauri nyota huyo aondoke katika klabu hiyo kwa lengo la kushinda mataji zaidi.

Gazeti la The Times linadai kwamba Spurs wamejawa na hofu kuwa Kane anaweza kufuata ushauri wa mshirika wake na kutimka katika klabu hiyo ifikapo mwezi Januari.

Mauricio Pochettino amekiri kuwa na mwanzo mgumu katika michuano ya msimu


Pochettino mwenyewe, pia hana uhakika wa kuendelea kukinoa kikosi hicho, huku cha Kaskazini mwa London, huku Real Madrid na Manchester United wakiwa miongoni mwa vilabu ambavyo vimekuwa vikimuwania kwa muda mrefu sana.
Spurs yahofia kumpoteza Harry Kane Spurs yahofia kumpoteza Harry Kane Reviewed by Zero Degree on 10/05/2019 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.