Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Oktoba 21, 2019
Chelsea imemuongeza aongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto.
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Express)
Manchester United inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. (Sun)
Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. (Chronicle)
Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. (Chronicle)
Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. (Telegraph)
Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 28, anasema angelijiunga na Everton msimu huu lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hakuridhishwa na ofa aliotolewa na klabu hiyo. (Het Laatste Nieuws)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. (Mail)
Alexandre Lacazette, 28 |
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. (Mail)
Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman angependelea kuwa msimamizi wa klabu ya Barcelona siku moja na anasema kuwa mkataba wake una kifungu cha sheria kinachomruhusu kuajiriwa na baada ya mashindano ya Ulaya mwaka 2020, amesema mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la kandanda la Uhuolanzi, Nico-Jan Hoogma.(Fox Sports)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Oktoba 21, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
10/21/2019 07:50:00 AM
Rating: