Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Oktoba 6, 2019


Manchester United wamekanusha taarifa inayodai kuwa Paul Pogba anadai kulipwa fidia ya pauni 600,000 kwa wiki kwenye mkataba mpya.

Sean Longstaff ameambiwa asahau kuhusu ndoto ya uhamisho wa pauni milioni 40 kwenda Manchester United.

Real Madrid wameingia katika hatua za mwisho kumsajili nyota wa klabu ya Ajax Donny van de Beek, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 100 - miezi mitatu ikiwa imepita tangu Manchester United waahirishe kumsajili kiungo huyo kwa robo tatu ya dau hilo. (Mirror)

Gareth Southgate atawaeleza kwa ufupi wachezaji wa Uingereza kipi cha kufanya pale watakapokumbana na vitenddo vya ubaguzi kwenye michezo ya kufuzu kushiriki michuano ya Euro 2020 dhidi ya Bulgaria. (Telegraph)

Hofu juu ya kuahirishwa kwa dili la ununuzi wa klabu ya Sunderland inazidi kuongezeka maradufu.

Nyota wa klabu ya Newcastle, Matt Ritchie amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu. (Stars)

Leicester wako kwenye msako wa mabeki wa kushoto, huku Ben Chilwell akitarajiwa kuondoka kwa pauni milioni 50.

Sheffield United wako tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili nyota wa klabu ya Brentford, Ollie Watkins.

Gary Rowett ni chaguo la kwanza la Millwall kuchukua nafasi ya Neil Harris kama meneja.

Brighton wanaandaa ofa ya pauni milioni 10 kumsajili beki wa klabu ya Preston Ben Davies.

Sheffield United wamejiandaa kutumia fedha za kutoshaare kumsajili nyota Ollie Watkins. (Sun)

Christian Pulisic

Christian Pulisic yuko tayari kufikiria juu ya hatima yake katika klabu ya Chelsea ifikapo mwezi Januari kama ataendelea kuwekwa benchi na kocha wa klabu hiyo Frank Lampard.

Jermain Defoe yuko kwenye mazungumzo na meneja wa Rangers Steven Gerrard kuhusu kusalia Ibrox kwa mkataba wa kudumu msimu ujao.

Steve Bruce anatarajiwa kuwachezesha ndugu wawili Sean na Matty Longstaff  katika kiungo kwenye mchezo wa Newcastle dhidi ya Manchester United.

Manchester United wako tayari kumteua mataalamu wa maumivu ya viungo wa Celtic Tim Williamson kufuatia mazungumzo yao kumalizika kwa mafanikio.

Millwall wana hamu ya kufanya mazungumzo na meneja wa Forest Green Rovers Mark Cooper kuhusu kuchukua nafasi ya Neil Harris.

Middlesbrough wanamnyemelea beki wa kulia wa klabu ya Kilmarnock Stephen O'Donnell. (Daily Mail)

Meneja mkuu wa Chelsea Frank Lampard anasema kuwa wachezaji wakubwa lazima wawe chachu kwa chipukizi. (Observer)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Oktoba 6, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Oktoba 6, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/06/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.